Hayo yalisemwa na Rais Mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akiahirisha Tamasha la 40 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni katika Viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASuBA) Wilayani Bagamoyo tarehe 30/10/2021.
Utamaduni ni Kielelezo cha Utashi na Uhai wa jamii na nchi kwa ujumla alisema Kikwete. Nimefurahishwa sana burudani ya ngoma lakini nimefurahi zaidi kwamba Tamasha hili limetumika kutangaza na kuhamasisha umma kutembelea Vivutio vya Utalii kama vile Magofu ya Kaole na Mjimkongwe"Kikwete". Alishauri na kusisitiza yafanyike maboresho hususan kwenye eneo ilipokuwa Bandari ya Kale Kaole na maeneo mengine ili kuvutia watalii zaidi. Akifungua Tamasha hilo tarehe 28/10/2021 Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo (WUSM) Mhe Innocent Bashungwa (Mb) alisema WUSM itawekeza zaidi kuhakikisha Sanaa na Utamaduni vinatumika kutangaza Vivutio vya Utalii vilivyopo nchini ili kuungana na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kupitia Royal Tour.